Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Penzi la Damu
Mstahamilivu hula
mbivu, mtaka cha uvunguni sharti ainame, na mchumia juani hulia
kivulini. Ni machache ya maadili yamuongozayo binti Malaika katika
safari yake ya kutimiza ndoto zake. Kujiendeleza kielimu ndiyo ndoto
yake kuu. Kwa vile Mungu hamtupi mja wake, anabahatika kwenda ughaibuni
kitaaluma. Ni safari inayomtenganisha na mpenzi wake, Ben. Lakini Ben
anaahidi kumsubiri hadi afuzu masomo yake. Katika kipindi hiki cha
utengano, dunia inawapangia mambo mengine kabisa, ni utengano unaotishia
kulisumu penzi lao. Majaribu hayeshi, vishawishi ni vingi. Penzi lao
linayumba, linatishia kudumbukia kwenye dimbwi la damu. Lakini Malaika
haliachii penzi lake kwa Ben, analipigania kishujaa. Ben pia anaingia
vitani kulipigania penzi la Malaika. Je, watashinda vita hivi vya
kimapenzi?
£16.00 – £17.00
About the author
Anna Manyanza ni
mwanafasihi wa riwaya na hekaya za watoto. Riwaya yake ya kwanza, ‘Penzi
La Damu’, imeshinda Tuzo ya Kiswahili ya Mabati -Cornell ya Fasihi ya
Afrika, mwaka 2015.