Pages: 104

Year: 2019

Category: Literature, Poetry

Dimensions: 229 x 152mm

ISBN:
Shipping class: POD

Machozi Yamenishiya

Mateso, maumivu na siasa ni mambo yaliyojaa uchochezi mkali unaomsukuma mshairi kuzungumza waziwazi na kinagaubaga na hatimaye kumfanya mwandishi apandwe na jazba zinazofanya kazi fulani itoke nje ya kingo za ulingo wa kisanaa. Katika hali kama hii mshairi lazima atunge wimbo unaoimbika ndani ya nafsi yake mwenyewe kwanza, wimbo utakaomwezesha kunyanyuka kitandani asubuhi huku akijua hayuko pweke, ana wenzake wenye maumivu kama au kuliko yake. Mohammed Khelef Ghassani ana weledi huu wa kubaki ndani ya kingo za ulingo wa kisanaa, weledi wa kuichenga siasa kwa namna ya kuipa nguvu kubwa zinazoficha na kuzimua unagaubaga na hata ukali wake.

Price range: £17.00 through £18.00

About the author

Mohammed Khelef Ghassani

Mohammed Khelef Ghassani alizaliwa mwaka 1977 visiwani Zanzibar na ni mwandishi wa diwani kadhaa za ushairi, zikiwemo Andamo: Msafiri Safarini, Siwachi Kusema: Uhuru U Kifungoni, Kalamu ya Mapinduzi: Mapambano Yanaendelea na N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini, ambayo ndiyo iliyompatia tuzo ya Fasihi ya Kiafrika kwa Lugha ya Kiswahili iliyotolewa na Mabati-Cornell mwaka 2015. Mbali na kuwa mshairi, Mohammed Ghassani ni mwandishi wa habari anayeishi na kufanya kazi zake nchini Ujerumani.

Related books

Penzi la Damu

Price range: £16.00 through £17.00

Mwanangu Rudi Nyumbani

Price range: £16.00 through £17.00

Mmeza Fupa

Price range: £17.00 through £18.00

Vitimbi vya Mama wa Kambo

£19.00

Mungu Hakopeshwi

Price range: £17.00 through £18.00