Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Pages: 212
Year: 2019
Category: Literature, Politics & Espionage
Dimensions: 198 x 129mm
Riwaya ya Mmeza Fupa ni riwaya iliyoshinda an kupewa tuzo ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika kwa mwaka 2017. Katika tangazo la ushindi wa riwaya hii jopo la majaji lilitoa sifa zifuatazo: Si mno mtu kukutana na riwaya ya Kiswahili ambayo mwandishi wake amejidhihirisha kuwa ni mbuji wa lugha fasaha na ya kisanii, inayotiririka kitabia kwa hiari yake, na bila ya kuonesha dalili zozote kwamba imelazimishwa. Wahusika wake wote wamebuniwa kwa ustadi, na kupewa kazi muwafaka za kuziwakilisha tanzu na matabaka mbalimbali ya jamii – pamoja na mikinzano na mazingira yao ya kihistoria, ya kisiasa,ya kisaikolojia, ya kitamaduni, ya kimjini au ya kijijini. Licha ya kwamba matukio ya riwaya hii yanatokea katika kisiwa cha kubuni, maswala yanayojadiliwa humu ni miongoni mwa yale maswala sugu yanayoendelea kulisumbua bara la Afrika kisiasa, kijamii na kiuchumi. Riwaya hii inatudhihirishia mandhari mapya ya utanzu huu wa Fasihi ya Kiswahili.
Uzito wa mivutano ya karne na migongano ya zama hubebwa migongoni mwa mwanadamu. Huchuana na wakati, katika kupapatuana na tsunami ya matendo ya mwanadamu. Ndivyo alivyoibuka Bi. Msiri kwenye joto la visasi, akaponea chupuchupu kumezwa na chatu-binadamu. Siku ya kuteketezwa kwa familia yake yeye alikuwa mtoni kufua. Aliporudi nyumbani alipokewa na simanzi nzito na rekecho la harufu ya damu. Hapo hapakumweka, huo ukawa mwanzo wa yeye kuwa mfungwa huru, akalimeza fupa ndani ya mapito ya karne mbili zilizompitia utosini. Kwa kuwa kwake mgubia chumvi nyingi chini ya jua, aliyajua mengi yaliyotiwa kapuni wakati ule. Akaweza kuja kuyasimulia wakati mwengine kwa vijana wengine aliowaamini.
Price range: £17.00 through £18.00
About the author
Ali Hilal ni mwandishi chipukizi aliyeibuka mitandaoni kwenye uandishi na hatimaye kuingia vitabuni. Ni mzaliwa wa Kisiwani Pemba, Zanzibar. Ni mwandishi anaeogelea bahari zote – Riwaya, hadithi fupi, ushairi na tamthilia. Miongoni mwa kazi zake zilizochapishwa ni Riwaya ya Safari yangu na Diwani ya Kurasa Mpya (Fungamano la Malenga).
Review
“In Mungu Hakopeshwi, Zainab Alwi Baharoon, has used the standard unguja Swahili masterfully. The language used flows so effortlessly that the reader can also have fun while reading. The overriding issue handled in this work is women’s struggles against the backdrop of male chauvinism and domination where the women find themselves at the bottom rung of the societal ladder (especially in the Swahili society).”
Mabati Cornell Kiswahili Prize