Publisher: Mkuki na Nyota Publishers, Tanzania
Pages: 162
Year: 2020
Category: Literature, Short Stories
Dimensions: 198 x 129mm
na hadithi nyingine
Vitimbi vya Mama wa Kambo, Wivu, Radhi za Wazazi, Ra ki Maluuni, Mchumba Kaka na Adui Mama ni hadithi zinazosawiri jamii alimochipukia mwandishi, au kuishi na kufanya kazi akiwa polisi, mwandishi wa habari na mtangazaji wa redio katika nchi za Tanzania, Rwanda, Burundi na Uingereza kwa takriban miaka 40. Kitabu hiki ni matokeo ya maombi ya watu wengi waliomsikiliza akizisimulia katika kipindi cha Hadithi na Muziki cha Redio Rwanda katika miaka ya 1980 na 1990. Hadithi hizi pia zimekuwa zikitumiwa na wakuza mitaala wa Kiswahili nchini Rwanda shuleni na zimewafurahisha wapenzi wengine wa fasihi nje ya shule.
£19.00
About the author
Ally Yusufu Mugenzi kwa jina jingine Ally Kayamba alijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania mwaka 1978. Alipohitimu mwaka 1980, aliajiriwa na Shirika la Habari Tanzania – SHIHATA. Mwaka 1983 aliacha kazi SHIHATA akajiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Rwanda. Mwanzoni mwa mwaka 1994, aliacha kazi Radio Rwanda alipoajiriwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC-London. Akiwa BBC, alianzisha idhaa ya kukutanisha watu waliotenganishwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda. Baadaye ilibadilika na kuwa Idhaa ya Maziwa Makuu. Mwaka 2005 aliteuliwa kuwa mhariri wa idhaa hiyo ambako yuko mpaka sasa.